Ijumaa ya 10 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
2Kor. 4:7 – 15Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya Imani; kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena; tukijua ya kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha pamoja nanyi. Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 116:10 – 11, 15 – 19Nitakutolea dhabihu ya kushukuru, Ee Bwana.
Naliamini, kwa maana nitasema,
Mimi naliteswa sana.
Mimi nalisema kwa haraka yangu,
Wanadamu wote ni waongo.
K. Nitakutolea dhabihu ya kushukuru, Ee Bwana.
Ina thamani machoni pa Bwana
Mauti ya wacha Mungu wake.
Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako,
Mtumishi wako, mwana na mjakazi wako,
Umevifungua vifungo vyangu.
K. Nitakutolea dhabihu ya kushukuru, Ee Bwana.
Nitakutolea dhabihu ya kushukuru;
Na kulitangaza jina la Bwana;
Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana,
Naam, mbele ya watu wake wote.
K. Nitakutolea dhabihu ya kushukuru, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
2Tim. 1:10Mwokozi wetu Yesu Kristu alibatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika kwa Injili.
Aleluya.
Injili
Mt. 5:27-32Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni