KUMBUKUMBU YA MT. BONIFASI (ASKOFU NA SHAHIDI)
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Tob. 1:1, 2:1-8Mimi Tobiti, nilipofika nyumbani kwangu, na kurudishiwa mke wangu Ana na mwanangu tobia, kwenye sikukuu ya Pentekoste, iliyo siku takatifu ya juma saba, naliandaliwa chakula kizuri, nikakaa kitako nile. Ndipo nilipoona nyama tele, nikamwambia mwanangu, Nenda ukamlete mtu maskini yeyote utakayemwona miongoni mwa ndugu zetu amkumbukaye Bwana. Haya! Nakungojea. Akarudi, akasema, Baba, kuna mtu mmoja wa taifa letu amenyongwa; akatupwa sokoni. Mara, kabla sijadiriki kuonja chakula chochote, naliondoka kwa haraka, nikaenda nikamchukua, nikampeleka katika chumba hata kuchwa kwa jua. Kisha nikarudi nikaoga, nikala chakula changu kwa msiba, huku nikiukumbuka ule unabii wa Amosi, kusema, Nitageuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio.
Kwa hiyo nikalia; na jua lilipokwisha kuchwa, nalikwenda nikachimba kaburi, nikamzika. Lakini jirani zangu walinidhihaki, wakasema, Mtu huyu bado haogopi kuuawa kwa sababu ya tendo hilo; ingawa alikimbia; na kumbe! Anazika maiti tena.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 112:1 – 6Heri mtu amchaye Bwana.
Aleluya.
Heri mtu yule amchaye Bwana,
Apendezwaye sana na maagizo yake.
Wazao wake watakuwa hodari duniani;
Kizazi cha Wenye adili kitabarikiwa.
K. Heri mtu amchaye Bwana.
Au: Aleluya.
Nyumbani mwake mna utajiri na mali,
Na haki yake yakaa milele.
Nuru huwazukia wenye adili gizani;
Ana fadhili na huruma na haki.
K. Heri mtu amchaye Bwana.
Au: Aleluya.
Heri atendaye fadhili na kukopesha;
Atengenezaye mambo yake kwa haki.
Kwa maana hataondoshwa kamwe;
Mwenye haki atakumbukwa milele.
K. Heri mtu amchaye Bwana.
Au: Aleluya.
Shangilio la Injili
Zab. 119:105Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.
Injili
Mk. 12:1-12Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni