Alhamisi ya 4 ya Kwaresima
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Kut 32:7-14Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 106:19-23Walifanya ndama huko Horebu, Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka.
Wakaubadili utukufu wao Kuwa mfano wa ng'ombe mla majani.
(K)Ee Bwana unikumbuke mimi, Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako
Wakamsahau Mungu, mwokozi wao, Aliyetenda makuu katika Misri.
Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu, Mambo ya kutisha penye bahari ya Shamu.
(K)Ee Bwana unikumbuke mimi, Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako
Akasema ya kuwa atawaangamiza Kama Musa, mteule wake, asingalisimama,
Mbele zake kama mahali palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaharibu.
(K)Ee Bwana unikumbuke mimi, Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako
Injili
Yn 5:31-47Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona. Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye. Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima. Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu. Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu. Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo. Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti? Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi. Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni