Jumatano ya 4 ya Pasaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo. 12:24-13:5Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.
Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro. Na walipokuwa katika Salami waklihubiri neno la Mungu katika masinagogi ya Wayahudi.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 67:1-2, 4, 5, 7Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.
Mungu na atufadhili na kutubariki,
Na kutuangazia uso wake.
Njia yake ijulikane duniani,
Wokovu wake katikati ya mataifa yote.
K. Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.
Au Aleluya.
Mataifa na washangilie,
Naam, waimbe kwa furaha,
Maana kwa haki utawahukumu watu,
Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
K. Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.
Au Aleluya.
Watu na wakushukuru, Ee Mungu,
Watu wote na wakushukuru.
Mungu atatubariki sisi;
Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.
K. Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.
Au Aleluya.
Shangilio la Injili
Yn. 10:14Mimi ndimi mchungaji mwema,
Nao walio wangu nawajua, nao walio wangu wanijua mimi.
Aleluya.
Injili
Yn. 12:44-50Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni