KUMBUKUMBU YA MT. YOSEFU, MFANYAKAZI
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mwa. 1 : 26-2 : 3Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 90:2-4, 12-14, 16Kazi ya mikono yetu uithibitishe, Ee Bwana
Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba duma,
Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
K. Kazi ya mikono yetu uithibitishe, Ee Bwana
Wamrudisha mtu mavumbini,
Usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
Maana miaka elfu machoni pako
Ni kama siku ya jana ikiisha kupita,
Na kama kesha la usiku.
K. Kazi ya mikono yetu uithibitishe, Ee Bwana
Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu,
Tujipatie moyo wa hekima.
Ee Bwana, urudi, hata lini?
Uwahurumie watumishi wako.
K. Kazi ya mikono yetu uithibitishe, Ee Bwana
Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,
Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote. Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako.
Na adhama yako kwa watoto wako.
K. Kazi ya mikono yetu uithibitishe, Ee Bwana
Injili
Mt. 13:54-48Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni