Alhamisi ya 5 ya Kwaresima
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mwa. 17:3-9Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzaqo wako kwa vizazi vyao baada yako.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 150: 4-9Analikumbuka agano lake milele.
Mtakeni Bwana na nguvu zake,
Utafuteni uso wake siku zote.
Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya,
Miujiza yake na hukumu za kinywa chake.
K. Analikumbuka agano lake milele.
Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake;
Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu;
Duniani mwote mna hukumu zake.
K. Analikumbuka agano lake milele.
Analikumbuka agano lake milele;
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
Agano alilofanya na Ibrahimu,
Na uapo wake kwa Isaka.
K. Analikumbuka agano lake milele.
Shangilio la Injili
2 Kor. 6:2Injili
Yn. 8:51-59Yesu akajibu, nikijutukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.
Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni