Alhamisi ya 1 ya Kwaresima
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Est. 4:17Bwana wangu, Wewe peke yako u Mfalme wetu. Unisaidie mimi niliye mkiwa, wala sina msaidizi wmingine ila Wewe; maana hatari yangu imo mkononi mwangu.
Tangu nilipozaliwa katika kabila ya jamaa yangu, nimesikia ya kuwa Wewe, Bwana, ulimchagua Israeli katika mataifa yote, na baba zetu katika jamaa zao, kuwa urithi wa daima, ukawatimilizia yote uliyoyaahidi.
Utukumbuke, Ee Bwana; ujifunue wakati wa taabu yetu; unipe moyo thabiti, Ee Mfalme wa miungu na Bwana wa milki zote. Unitie kinywani mwangu maneno ya kufaa mbele ya samba, ukaugeuza moyo wake apate kumchukia yule anayepigana nasi, ili akomeshwe pamoja na wote wenye nia moja naye. Lakini utuokoe sisi kwa mkono wako; unisaidie mimi niliye peke yangu, bila msaidizi mwingine ila Wewe, Bwana.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 138:1-3, 8-9Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu,
Nitalishukuru jina lako.
K. Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,
Kwa amana umeikuza ahadi yako,
Kuliko jina lako lote.
Siku ile niliyokuita uliniitikia,
Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
K. Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
Na mkono wako wa kuume utaniokoa.
Bwana atanitimilizia mambo yangu;
Ee Bwana, fadhili zako ni za milele;
Usiziache kazi za mikono yako.
K. Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
Shangilio la Injili
Eze. 33:11Injili
Mt. 7:7-12Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hivyo ndiyo torati na manabii.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni