Sherehe ya Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni.
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Ufu 11: 19, 12: 1-6, 10Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 45: 9-11, 15Mkono wako wa kuume amesimama malkia. amevaa dhahabu ya Ofiri.
Binti za wafalme wamo
Miongoni mwa akina bibi wako wastahiki.
Mkono wako wa kuume amesimama malkia,
Amevaa dhahabu ya Ofiri.
Sikia, binti, utazame, utege sikio lako,
Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako.
K. Mkono wako wa kuume amesimama malkia. amevaa dhahabu ya Ofiri.
Naye mfalme atautamani uzuri wako,
Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie.
Watapelekwa kwa furaha na shangwe,
Na kuingia katika nvumba va mfalme.
K. Mkono wako wa kuume amesimama malkia. amevaa dhahabu ya Ofiri.
Somo la Pili
1Kor 15: 20-26Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
ShangilioMaria amepalizwa mbinguni majeshi yote ya malaika wanafurahi.
Aleluya.
Injili
Lk 1: 39-56Mariamu akasema,
Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
Na roho yangu imemfurahia Mungu,
Mwokozi wangu;
Kwa kuwa ameutazama
Unyonge wa mjakazi wake.
Kwa maana, tazama, tokea sasa
Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;
Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu,
Na jina lake ni takatifu.
Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi
Kwa hao wanaomcha.
Amefanya nguvu kwa mkono wake;
Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi;
Na wanyonge amewakweza.
Wenye njaa amewashibisha mema
Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu.
Amemsaidia Israeli, mtumishi wake;
Ili kukumbuka rehema zake;
Kama alivyowaambia baba zetu,
Ibrahimu na uzao wake hata milele.
Mariamu akakaa naye kadiri ya miezi mitatu, kisha akarudi kwenda nyumbani kwake.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni