Jumatatu ya 17 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer 13:1–11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Kumb 32:18–21Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa.
Hukumbuki Mwamba aliyekuza,
Mungu aliyekuzaa umemsahau.
Bwana akaona, akawachukia,
Kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake.
K. Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa.
Akasema, nitawaficha uso wangu,
Nitaona mwisho wao utakuwaje;
Maana, ni kizazi cha ukaidi mwingi,
Watoto wasio imani ndani yao.
K. Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa.
Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu,
Wamenikasirisha kwa ubatili wao;
Nami nitawatia wivu kwa wasio watu.
Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo.
K. Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa.
Shangilio la Injili
Kol 16:17Neno la Kristu likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkimshukuru Mungu Baba kwa Yeye.
Aleluya.
Injili
Mt 13:31–35Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni