Kumbukumbu ya Mtakatifu Bonaventura, Askofu na Mwalimu wa Kanisa
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 10:5–7, 13–16Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti. Kwa hiyo Bwana, Bwana wa majeshi, atawapekelea kukonda watu wake walionona; na badala ya utukufu wake kutawashwa kuteketea kama kuteketea kwa moto.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 94:5–10, 14–15Bwana hatawatupa watu wake.
Ee Bwana, wanawaseta watu wako;
Wanauseta urithi wako;
Wanamwua mjane na mgeni;
Wanawafisha yatima.
K. Bwana hatawatupa watu wake.
Nao husema, Bwana haoni;
Mungu wa Yakobo hafikiri.
Enyi wajinga miongoni mwa watu fikirini;
Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili?
K. Bwana hatawatupa watu wake.
Aliyelitia sikio mahali pake asisikie?
Aliyelifanya jicho asilione?
Awaadhibuye mataifa asikemee?
Amfundishaye mwanadamu asijue?
K. Bwana hatawatupa watu wake.
Kwa kuwa Bwana hatawatupa watu wake.
Wala hutauacha urithi wake,
Maana hukumu itairejea haki,
Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata.
K. Bwana hatawatupa watu wake.
Shangilio la Injili
Zab 27:11Ee Bwana, unifundishe njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.
Injili
Mt 11:25–27Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni