Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Kum 7:6-11Basi, jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu; naye huwalipa wamchukiao mbele ya uso wao, ili kuwangamiza. Hatakuwa mlegevu kwake yeye amchukiaye, atamlipa mbele ya uso wake. Basi zishike amri, na sheria, na hukumu ninazoamuru leo, uzitende.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 103:1–4, 6–8, 10Fadhili za Bwana zina wamchao, tangu milele hata milele.
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Naam, vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi jina lake takatifu.
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Wala usizisahau fadhili zake zote.
K. Fadhili za Bwana zina wamchao, tangu milele hata milele.
Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,
Aukomboa uhai wako na kaburi,
Akutia taji ya fadhili na rehema.
K. Fadhili za Bwana zina wamchao, tangu milele hata milele.
Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki,
Na hukumu kwa wote wanaoonewa.
Alimjulisha Musa njia zake,
Wana wa Israeli matendo yake.
K. Fadhili za Bwana zina wamchao, tangu milele hata milele.
Bwana amejaa huruma na neema,
Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.
Hakututenda sawasawa na hatia zetu,
Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.
K. Fadhili za Bwana zina wamchao, tangu milele hata milele.
Somo la Pili
1Yoh 4:7–16Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Mt 11:29Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo.
Aleluya.
Injili
Mt 11:25-30Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
BAYIZI CHALRES · 13 Juni 2026
Tumusifu yesu kristu