KUMBUKUMBU YA WATAKATIFU TIMOTHEO NA TITO, MAASKOF
· Mwaka A
Somo la Kwanza
2 Tim. 1:1-8Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana. Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha; nikiikumbuka Imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.
Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yao kwa kuwekewa mikono yangu. Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu nay a upendo nay a moyo wa kiasi. Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 16:1-2, 5, 7-8, 11Bwana ndiye fungu la posho langu.
Mungu, unihifadhi mimi,
Kwa maana nakukimbilia Wewe.
Nimemwambia Bwana, Ndiwe Bwana wangu,
Sina wema ila utokao kwako.
K. Bwana ndiye fungu la posho langu.
Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri,
Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.
Nimemweka Bwana mbele yangu daima,
Kwa kuwa yako kuumeni kwangu, sitaondoshwa.
K. Bwana ndiye fungu la posho langu.
Utanijulisha njia ya uzima,
Mbele za uso wako iko furaha tele,
Na katika mkono wako wa kuume
Mna mema ya milele
K. Bwana ndiye fungu la posho langu.
Shangilio la Injili
Mt. 28:19-20Enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, Bwana anasema. Mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Aleluya.
Injili
Lk. 10:1-9Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni