Alhamisi ya 25 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Hag 1:1-8Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 149:1-6, 9Bwana awaridhia watu wake.
Aleluya,
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Sifa zake katika kusanyiko la watauwa!
Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya,
Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao!
K. Bwana awaridhia watu wake.
Na walisifu jina lake kwa kucheza,
Kwa matari na kinubi wamwimbie!
Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake,
Huwapamba wenye upole kwa wokovu.
K. Bwana awaridhia watu wake.
Watauwa na waushangilie utukufu,
Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao,
Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.
K. Bwana awaridhia watu wake.
Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa:
Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote.
K. Bwana awaridhia watu wake.
Shangilio la Injili
Zab 27:11Ee Bwana, unifundishe njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.
Injili
Lk 9:7–9Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni