Sikukuu ya Mt. Maria Magdalena
· Mwaka C · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Wim 3:1-4Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 63: 1-5, 7-8Nafsi yangu inakuonea kiu, Ee Bwana.
Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea kiu,
Mwili wangu wakuonea shauku,
Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
K. Nafsi yangu inakuonea kiu, Ee Bwana.
Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,
Nizione nguvu zako na utukufu wako.
Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai;
Midomo yangu itakusifu.
K. Nafsi yangu inakuonea kiu, Ee Bwana.
Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;
Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono;
Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
K. Nafsi yangu inakuonea kiu, Ee Bwana.
Maana Wewe umekuwa msaada wangu,
Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
Nafsi yangu inakuandama sana;
Mkono wako wa kuume unanitegemeza.
K. Nafsi yangu inakuonea kiu, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
ShangilioMaria tuambie: sema uliyoona njiani. Kaburi lilimfadhi yule aliye Mzima; Niliona utukufu wa Kristu alipokuwa akifufuka.
Aleluya.
Injili
Yn 20:1-2, 11-18Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni