KUMBUKUMBU YA WATAKATIFU BASILI MKUU NA GREGORI WA
· Mwaka A
Somo la Kwanza
1Yn 2:22-28Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza. Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake. Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake katika kuja kwake.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 98:1-4Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono wa kuume wake mwenyewe,
Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
K. Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
Bwana ameufunua wokovu wake,
Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
Amezikumbuka rehema zake,
Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli.
K. Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
Miisho yote ya dunia imeuona,
Wokovu wa Mungu wetu.
Mshangilieni Bwana, nchi yote,
Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
K. Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
Shangilio la Injili
ShangilioSiku takatifu imetung’aria: Enyi mataifa njoni mkambwabudu Bwana: Kwa sababu mwanga mkubwa umeshuka duniani.
Aleluya.
Injili
Yn. 1:19-28Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni