SIKUKUU YA FAMILIA TAKATIFU YA YESU, MARIA NA YOSE
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Ybs. 3:2-6, 12-14Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 128:1-5Heri kila mtu amchaye Bwana, aendaye katika njia zake.
Heri kila mtu amchaye Bwana,
Aendaye katika njia zake.
Taabu ya mikono yako hakika utaila;
Utakuwa heri, na kwako kwema.
K. Heri kila mtu amchaye Bwana, aendaye katika njia zake.
Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,
Vyumbani mwa nyumba yako.
Wanao kama miche ya mizeituni,
Wakiizunguka meza yako.
K. Heri kila mtu amchaye Bwana, aendaye katika njia zake.
Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana,
Bwana akakubariki toka Sayuni.
Uone uheri wa Yerusalemu,
Siku zote za maisha yako.
K. Heri kila mtu amchaye Bwana, aendaye katika njia zake.
Somo la Pili
Kol. 3:12-21Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana. Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Kol. 3:15,16Na Amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu.
Aleluya.
Injili
Mt. 2:13-15, 19-23Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto. Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli. Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya, akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni