Alhamisi Kuu
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Kut 12:1-8, 11-14Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 116:12-13, 15-18Kikombe kile cha Baraka tukibarikicho, Je! Si ushirika wa damu ya Kristo?
Nimrudishie Bwana nini
Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
Nitakipokea kikombe cha wokovu;
Na kulitangaza jina la Bwana.
K. Kikombe kile cha Baraka tukibarikicho, Je! Si ushirika wa damu ya Kristo?
Ina thamani machoni pa Bwana,
Mauti ya wacha Mungu wake.
Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako,
Mtumishi wako, mwana na mjakazi wako.
Umevifungua vifungo vyangu.
K. Kikombe kile cha Baraka tukibarikicho, Je! Si ushirika wa damu ya Kristo?
Nitakutolea dhabihu ya kushukuru;
Na kulitangaza jina la Bwana;
Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana,
Naam, mbele ya watu wake wote.
K. Kikombe kile cha Baraka tukibarikicho, Je! Si ushirika wa damu ya Kristo?
Somo la Pili
1Kor 11:23-26Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Yn 13:34Injili
Yn 13:1-15Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye. Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami. Simony Petro akamwambia, Bwana, si miguu yang utu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia. Yesu akamwambia, yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote. Kwa maana alimjua yeye atayemsaliti; ndiyo maana alisema, Si nyote mlio safi.
Basi alipkwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavzi yake, na kuteti tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea? Ninyi mwaniita Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni