Jumanne ya 5 ya Kwaresima
· Mwaka C · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Hes 21:4-9Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 102:1-2, 15-20Ee Bwana, usikie kuomba kwangu, kilio changu kikufikie.
Ee Bwana, usikie kuomba kwangu,
Kilio change kikufikie,
Usinifiche uso wako siku ya shida yangu,
Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi.
K. Ee Bwana, usikie kuomba kwangu, kilio changu kikufikie.
Kisha mataifa wataliogopa jina la Bwana,
Na wafalme wote wa dunia utukufu wako;
Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni,
Atakapoonekana katika utukufu wake,
Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa,
Asiyadharau maombi yao.
K. Ee Bwana, usikie kuomba kwangu, kilio changu kikufikie.
Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo,
Na watu watakaoumbwa watamsifu Bwana.
Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu,
Toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi,
Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa,
Na kuwafungua walioandikiwa kufa.
K. Ee Bwana, usikie kuomba kwangu, kilio changu kikufikie.
Shangilio la Injili
Yn 8:12Injili
Yn 8:21-30Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni