Kumbukumbu ya Mtakatifu Skolastika, Bikira
· Mwaka C · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mwa 1:1–19Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 104:1–2, 5–6, 10, 12, 24, 35Bwana na ayafurahie matendo yake.
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Wewe, Bwana, Mungu wangu, umejifanya mkuu sana.
Umejivika heshima na adhama,
Umejivika nuru kama vazi.
K. Bwana na ayafurahie matendo yake.
Uliiweka juu ya misingi yake,
Isitikisike milele,
Uliifunika kwa vilindi kama kwa vazi,
Maji yalikuwa yakisimama juu ya milima.
K. Bwana na ayafurahie matendo yake.
Hupeleka chemchemi katika mabonde;
Zapita kati ya milima,
Kando kando hukaa ndege wa angani,
Kati ya matawi hutoa sauti zao.
K. Bwana na ayafurahie matendo yake.
Ee Bwana, jinsi yalivyo mengi matendo yako!
Kwa hekima umevifanya vyote pia,
Dunia imejaa mali zako.
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
K. Bwana na ayafurahie matendo yake.
Shangilio la Injili
Zab 111:7, 8Maagizo yako yote, ee Bwana, ni amini, yamethibitika milele na milele.
Aleluya.
Injili
Mt 6:53-56Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni