Jumatano ya 2 ya Majilio
· Mwaka C · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 40:25-31Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, Bwana asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie? Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Haya vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 103:1-4, 8, 10Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Naam, vyote vilivyo ndani yangu,
Vilihimidi jina lake takatifu.
Ee nafsi yangu umhimidi Bwana,
Wala usizisahau fadhili zake zote.
K. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,
Aukomboa uhai wako na kaburi,
Akutia taji ya fadhili na rehema.
K. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Bwana amejaa huruma na neema,
Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.
Hakututenda sawasawa na hatia zetu.
Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.
K. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Shangilio la Injili
ShangilioTazama Bwana atakuja kuwaokoa watu wake, Heri walio tayari kumlaki.
Aleluya.
Injili
Mt 11:28-30Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni