Dominika ya 1 ya Majilio
· Mwaka C · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer 33:14-16Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 25:4-5, 8-9,10,14Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu.
Ee Bwana, unijulishe njia zako,
Unifundishe mapito yako,
Uniongoze katika kweli yako,
Na kunifundisha.
K. Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu.
Bwana yu mwema, mwenye adili,
Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.
Wenye upole atawaongoza katika hukumu,
Wenye upole atawafundisha njia yake.
K. Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu.
Njia zote za Bwana ni fadhili na kweli,
Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.
Siri ya Bwana iko kwao wamchao.
Naye atawajulisha agano lake.
K. Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu.
Somo la Pili
1Thes 3:12; 4:1-2Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Zab 85:7Ee Bwana utuonyeshe rehema zako, Utupe wokovu wako.
Aleluya.
Injili
Lk 21:25-28, 34-36Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo; kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
DAVID ELIA · 1 Desemba 2024
Amina!