Dominika ya 30 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer 31:7-9Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 126Bwana alitutendea mambo makuu, tulikuwa tukifurahi.
Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni,
Tulikuwa kama waotao ndoto.
Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko,
Na ulimi wetu kelele za furaha.
K. Bwana alitutendea mambo makuu, tulikuwa tukifurahi.
Ndipo mataifa waliposema,
Bwana amewatendea mambo makuu,
Bwana alitutendea mambo amkuu,
Tulikuwa tukifurahi.
K. Bwana alitutendea mambo makuu, tulikuwa tukifurahi.
Ee, Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, kama vijito vya Kusini.
Wapandao kwa machozi,
Watavuna kwa kelele za furaha.
K. Bwana alitutendea mambo makuu, tulikuwa tukifurahi.
Ingawa mtu anakwenda zake akilia,
Azichukuapo mbegu za kupanda.
Hakika atarudi kwa kelele za furaha,
Aichukuapo miganda yake.
K. Bwana alitutendea mambo makuu, tulikuwa tukifurahi.
Somo la Pili
Ebr 5:1-6Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Ef 1:17-18Ewe Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, uyatie nuru macho ya mioyo yetu, ili tujue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo.
Aleluya.
Injili
Mk 10:46-52Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Edmond Wafula · 27 Oktoba 2024
Ningependa kuchukua nafasj hii kuwashukuru nyote mliohusika katika kufanikisha website hii... Kwa kweli, mkatoliki leo inatosha .. napata mafunzo n masomo kabla ya ibaada kuanza