SIKUKUU YA UKULU WA MT. PETRO (MTUME)
· Mwaka C
Somo la Kwanza
1 Pet. 5:1-4Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 23 (K) 1Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Bwana ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Huniuisha nafsi yangu, na kuniongoza,
Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Naam nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya,
Kwa maana wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Hakika wema na fadhili zitanifuata,
Siku zote za maisha yangu,
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Injili
Mt. 16:13-19Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni