Alhamisi ya 15 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 26:7–9, 12, 16–19Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 102:12–20Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Wewe, Bwana, utaketi ukimiliki milele,
Na kumbukumbu lako kizazi hata kizazi.
Wewe mwenyewe utasimama,
Na kuirehemu Sayuni,
Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia,
Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia.
Maana watumishi wake wameyaridhia mawe yake;
Na kuyaonea huruma mavumbi yake.
K. Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Kisha mataifa wataliogopa jina la Bwana,
Na wafalme wote wa dunia utukufu wake.
Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni,
Atakapoonekana katika utukufu wake.
Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa,
Asiyadharau maombi yao.
K. Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Kizazi kitakachokuja kitaandikia hayo,
Na watu watakaoumbwa watamsifu Bwana.
Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu,
Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa,
Na kuwafungua walioandikiwa kufa.
K. Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Shangilio la Injili
Zab 111:7, 8Maagizo yako yote, ee Bwana, ni amini, yamethibitika milele na milele.
Aleluya.
Injili
Mt 11:28–30Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni