Ijumaa ya 12 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
2Fal 25:1-12Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 137:1-6Ulimi wangu ugandamane nisipokukumbuka
Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi,
Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.
Katika miti iliyo katikati yake
Tulivitundika vinubi vyetu.
K. Ulimi wangu ugandamane nisipokukumbuka
Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie;
Na waliotuonea walitaka furaha;
Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.
K. Ulimi wangu ugandamane nisipokukumbuka
Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni?
Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe,
Mkono wangu wa kuume na usahau.
K. Ulimi wangu ugandamane nisipokukumbuka
Ulimi wangu na ugandamane
Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka.
Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu.
K. Ulimi wangu ugandamane nisipokukumbuka
Shangilio la Injili
Mt 8:17Kristu aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.
Aleluya
Injili
Mt 8:1-4Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni