Kumbukumbu ya Mt Antoni wa Padua, Padre na Mwalimu wa Kanisa
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Fal 18:41-46Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 65:9-12Ee Mungu, sifa zakulaki katika Sayuni.
Umeijilia nchi na kuisitawisha.
Umeitajirisha sana;
Mto wa mungu umejaa maji;
Wawaruzuku watu nafaka,
Maana ndiwe uitengenezaye ardhi.
K. Ee Mungu, sifa zakulaki katika Sayuni.
Matuta yake wayajaza maji;
Wapasawazisha palipoinuka,
Wailainisha nchi kwa manyunyu;
Waibariki mimea yake.
K. Ee Mungu, sifa zakulaki katika Sayuni.
Umeuvika mwaka taji ya wema wako;
Mapito yako yadondoza unono.
Huyadondokea malisho ya nyikani,
Na vilima vyajifunga furaha.
K. Ee Mungu, sifa zakulaki katika Sayuni.
Shangilio la Injili
Kol 3:16,17Neno la Kristo likaa kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Aleluya.
Injili
Mt 5:20-26Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue; na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kasha urudi uitoe sadaka yako. Patina na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni