Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Kristo
· Mwaka B
Somo la Kwanza
Hos. 11 : l, 3-4, 8-9Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja. Sitatumia ukali wa hasira yangu, sitarudi kumvvangamiza Efraimu; kwa maana mimi ni Mungu, si mwanadamu mimi; mimi ndiye aliye Mtakatifu katikati yenu; wala sitaingia ndani ya mji.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Isa. 12:2-6Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;
Nitatumaini wala sitaogopa;
Maana Bwana Yehova ni nguvu zangu na wimbo wangu;
Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
K. Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
Na katika siku hiyo mtasema,
Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake;
Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa,
Litajeni jina lake kuwa limetukuka.
K. Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
Mwimbieni Bwana, kwa kuwa ametenda makuu;
Na yajulikane haya katika dunia yote.
Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;
Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
K. Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
Somo la Pili
Efe. 3: 8-12, 14-19Kwa hiyo nampigia Baba magoti, ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu. Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya marnbo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
1 Yoh. 4:10Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeyc alitupenda sisi, akatuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.
Aleluya.
Injili
Yn. 19:31-37Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni