Jumanne ya 5 ya Pasaka
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo 14:19-28Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 145:10-13, 21Watawajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari wa zamani zote.
Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako,
Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
K. Watawajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari wa zamani zote.
Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
K. Watawajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari wa zamani zote.
Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana;
Wote wenye mwili na walihimidi jina lake
takatifu milele na milele.
K. Watawajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari wa zamani zote.
Shangilio la Injili
Ufu 1:5Ee Kristo, yu shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia.
Aleluya.
Injili
Yn 14:27-31Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Martin Muteti · 30 Aprili 2024
Tumshukuru mungu