Dominika ya 3 ya Pasaka
· Mwaka B · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo. 3:13-15, 17-19aBasi sasa, ndugu, najua ya kuwa mliyatenda haya kwa kutokujua kwenu, kama na wakuu wenu walivyotenda. Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo. Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 4:1,3,6,8Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo;
Umenifanyizia nafasi wakati wa shida;
Unifadhili na kuisikia sala yangu.
K. Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Au: Aleluya.
Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa;
Bwana atasikia nimwitapo.
K. Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Au: Aleluya.
Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema?
Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
K. Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Au: Aleluya.
Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara,
Maaana Wewe, Bwana, peke yako,
Ndiwe unijaliaye kukaa salama.
K. Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Au: Aleluya.
Somo la Pili
1Yoh. 2:1-5aNa katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Lk. 24:32Bwana Yesu, utufunulie maandiko; uwashe mioyo yetu unaposema nasi.
Aleluya.
Injili
Lk. 24:35-48Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu. Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho. Akawaambia, Mbona manafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo. Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula chochote? Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. Akakitwaa, akala mbele yao.
Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii, na Zaburi. Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu, na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo hayo.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni