Jumatano ya 2 ya Pasaka
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo 5:17-26Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 34:1-8Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.
Nitamhimidi Bwana kila wakati,
Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
Katika Bwana nafsi yangu itajisifu,
Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.
K. Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.
Mtukuzeni Bwana pamoja nami,
Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
Nalimtafuta Bwana akanijibu,
Akaniponya na hofu zangu zote.
K. Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.
Wakamwelekea macho wakatiwa nuru,
Wala nyuso zao hazitaona haya.
Maskini huyu aliita, Bwana akasikia,
Akamwokoa na taabu zake zote.
K. Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.
Malaika wa Bwana hufanya kituo,
Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema;
Heri mtu yule anayemtumaini.
K. Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.
Shangilio la Injili
Rum 6:9Kristo akiisha kufufuka, katika wafu hafi tena. Mauti haimtawali tena.
Aleluya.
Injili
Yn 3:16-21Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Martin Muteti · 10 Aprili 2024
Eeh Mungu tujalie wema wako tutembee kwenye nuru yako daima
Martin Muteti · 10 Aprili 2024
Amina