Kumbukumbu ya Wat. Paulo Miki na wenzake Mashahidi
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Fal 8:22-23, 27-30Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 84:2-4, 9-10Maskani zako zapendeza kama nini, ee Bwana wa majeshi.
Nafsi yangu imezionea shauku nyua za Bwana,
Naam, na kuzikondea.
Moyo wangu na mwili wangu
Vinamlilia Mungu aliye hai.
K. Maskani zako zapendeza kama nini, ee Bwana wa majeshi.
Shomoro naye ameona nyumba,
Na mbayuwayu amejipatia kiota,
Alipoweka makinda yake:
Kwenye madhabahu zako, ee Bwana wa majeshi,
Mfalme wangu na Mungu wangu.
K. Maskani zako zapendeza kama nini, ee Bwana wa majeshi.
Heri wakao nyumbani mwako,
Wanakuhimidi daima.
Ee Mungu, ngao yetu, uangalie,
Umtazame uso masihi wako.
K. Maskani zako zapendeza kama nini, ee Bwana wa majeshi.
Hakika siku moja katika nyua zako
Ni bora kuliko siku elfu.
Ningependa kuwa bawabu
Nyumbani mwa Mungu wangu,
Kuliko kukaa katika hema za uovu.
K. Maskani zako zapendeza kama nini, ee Bwana wa majeshi.
Shangilio la Injili
Zab 118:36, 29Unielekeze moyo wangu na shuhuda zako, na unineemeshe kwa sheria yako.
Aleluya.
Injili
Mk 7:1-13Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni