Sikukuu ya Yohane, Mtume na Mwinjili
· Mwaka B
Somo la Kwanza
1Yoh 1:1–4Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 97:1–2, 5–6, 11–12Enyi wenye haki, mfurahieni Bwana.
Bwana ametamalaki, nchi na ishangilie,
Visiwa vingi na vifurahi.
Mawingu na giza vyamzunguka,
Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.
K. Enyi wenye haki, mfurahieni Bwana.
Milima iliyeyuka kama nta mbele za Bwana,
Mbele za Bwana wa dunia yote.
Mbingu zimetangaza haki yake,
Na watu wote wameuona utukufu wake.
K. Enyi wenye haki, mfurahieni Bwana.
Nuru imemzukia mwenye haki,
Na furaha wanyofu wa moyo.
Enyi wenye haki, mfurahieni Bwana,
Na kulishukuru jina lake takatifu.
K. Enyi wenye haki, mfurahieni Bwana.
Shangilio la Injili
ShangilioEe Mungu, tunakusifu, tunakukiri kuwa Bwana. Jamii tukufu ya Mitume inakusifu.
Aleluya.
Injili
Yn 20:2–8Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni