Alhamisi ya 1 ya Majilio
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 26:1-6Mtumainini Bwana sikuzote, maana Bwana Yehova ni mwamba wa milele. Kwa kuwa amewashusha wakaao juu, mji ule ulioinuka, aushusha, aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini. Mungu utaukanyaga chini, naam, miguu yao walio maskini, na hatua zao walio wahitaji.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 118:1, 8-9, 19-21, 25-27aNa abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana.
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema
Kwa maana fadhili zak eni za milele,
Ni heri kumkimbilia Bwana,
Kuliko kuwatumainia wanadamu,
Ni heri kumkimbilia Bwana
Kuliko kuwatumainia wakuu.
K. Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana.
Nifungulieni malango ya haki,
Nitaingia na kumshukuru Bwana.
Lango hili ni la Bwana,
Wenye haki ndio watakaoliingia.
Nitakushukuru kwa maana umenijibu,
Nawe umekuwa wokovu wangu.
K. Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana.
Ee Bwana, utuokoe, twakusihi,
Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana,
Tumewabarikia toka nyumbani mwa Bwana.
Bwana ndiye aliye Mungu,
Naye ndiye aliyetupa nuru.
K. Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana.
Shangilio la Injili
Isa 55:6Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni maadamu yu karibu.
Aleluya.
Injili
Mt 7:21, 24-27Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni