Jumatatu ya 32 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Hek 1:1-7Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 139:1-10Uniongoze katika njia ya milele, Ee Bwana.
Ee Bwana umenichunguza na kunijua.
Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;
Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,
Umeelewa na njia zangu zote.
K. Uniongoze katika njia ya milele, Ee Bwana.
Maana hamna neno ulimini mwangu
Usilolijua kabisa, Bwana.
Umenizingira nyuma na mbele,
Ukaniwekea mkono wako.
Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi,
Hayadirikiki, siwezi kuyafikia.
K. Uniongoze katika njia ya milele, Ee Bwana.
Niende wapi nijiepushe na roho yako?
Niende wapi niukimbie uso wako?
Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko,
Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
K. Uniongoze katika njia ya milele, Ee Bwana.
Ningezitwaa mbawa za asubuhi,
Na kukaa pande za mwisho za bahari;
Huko nako mkono wako utaniongoza,
Na mkono wako wa kuume utanishika.
K. Uniongoze katika njia ya milele, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
2Kor 5:19Mungu alikuwa ndani ya Kristu, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Aleluya.
Injili
Lk. 17:1 – 6Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni