Ijumaa ya 28 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Rum 4:1-8Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 32:1-2.5.11Ni wewe sitara yangu, Ee Bwana.
Heri aliyesamehewa dhambi,
Na kusitiriwa makossa yake.
Heri Bwana asiyemhesabia upotovu,
Ambaye rohoni mwake hamna hila.
K. Ni wewe sitara yangu, Ee Bwana.
Nalikujulisha dhambi yangu,
Wala sikuuficha upotovu wangu.
Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa Bwana,
Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
K. Ni wewe sitara yangu, Ee Bwana.
Mfurahieni Bwana;
Shangilieni, enyi wenye haki.
Pigeni vigelegele vya furaha;
Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.
K. Ni wewe sitara yangu, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
Zab. 130:5Roho yangu inamngoja Bwana, na neno lake nimelitumainia.
Aleluya.
Injili
Lk. 12:1-7Name nawaambia ninyi rafiki zangu, msiwaogope hao wauuao mwili, kisha baada ya hayo hawana wawezalo kutenda Zaidi. Lakini nitawaonya mtakayemwogopa, mwogopeni yule ambaye akiishakumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanam; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo. Je! Mashomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu. Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi, bora ninyi kuliko mashomoro wengi.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni