Ijumaa ya 21 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
1 The 4: 1-8Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 97:1-2, 5-6, 10-12Enyi wenye haki, mfurahini Bwana.
Bwana ametamalaki, nchi na ishangilie,
Visiwa vingi na vifurahi.
Mawingu na giza vyamzunguka,
Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.
K. Enyi wenye haki, mfurahini Bwana.
Milima iliyeyuka kama nta mbele za Bwana,
Mbele za Bwana wa dunia yote.
Mbingu zimetangaza haki yake,
Na watu wote wameuona utukufu wake.
K. Enyi wenye haki, mfurahini Bwana.
Enyi mpendao Bwana, uchukieni uovu;
Huwalinda nafsi zao watauwa wake,
Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.
K. Enyi wenye haki, mfurahini Bwana.
Nuru imemzukia mwenye haki,
Na furaha wanyofu wa moyo.
Enyi wenye haki, mfurahieni Bwana,
Na kulishukuru jina lake takatifu.
K. Enyi wenye haki, mfurahini Bwana.
Shangilio la Injili
Yn 15: 15Bwana anasema: Siwaiti tena watumwa, lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifa.
Aleluya.
Injili
Mt 25: 1-13Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni