Sikukuu ya Mtakatifu Bartlomeo, Mtume
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ufu 21: 9-14Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 145: 10-13, 17-18Wacha Mungu wataunena,
Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Wataunena utukufu wa ufalme wako,
na kuuhadithia uweza wako.
K. Wacha Mungu wataunena,
utukufu wa ufalme wako, Ee Bwana.
Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
K. Wacha Mungu wataunena,
utukufu wa ufalme wako, Ee Bwana.
Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote,
Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.
Bwana yu karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa uaminifu.
K. Wacha Mungu wataunena,
utukufu wa ufalme wako, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
Yn 1: 49Rabi, wewe u Mwana wa Mungu,
ndiwe Mfalme wa Israeli.
Aleluya.
Injili
Yn 1: 45-51Basi Yesu, akamwona Nathanaeli anakuja kwa- ke, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli. Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. Akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu waki- kwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni