Jumamosi ya 18 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kum. 6: 4-13Tena itakuwa atakapokwisha Bwana, Mungu wako, kukuleta katika nchi aliyowaapia babu zako, Ibrahimu na Isaka na Yakobo, ya kuwa atakupa; miji mikubwa mizuri usiyoijenga wewe, na nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza wewe, na visima vimefukuliwa usivyofukua wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba; ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana alivekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa. Mche Bwana, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 18 :1-2, 46, 50Wewe Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana.
Wewe, Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana;
Bwana ni jabali langu, na boma langu,
na mwokozi wangu.
K. Wewe Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana.
Bwana ndiye aliye hai;
Na ahimidiwe mwamba wangu;
Na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu.
K. Wewe Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana.
Ampa mfalme wake wokovu mkuu,
Amfanyia fadhili masihi wake,
Daudi na mzao wake hata milele.
K. Wewe Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana.
Shangilio la Injili
Yn. 8: 12Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana,
yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,
bali atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.
Injili
Mt. 17: 14-20Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema, Mbona sisi hatukuweza ku- mtoa? Yesu akawaambia, Kwa sababu va upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni