Kumbukumbu ya Mtakatifu Yohane Maria Vianney
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Law. 23 :1, 4-11,15-16,27, 34-37Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi. Lakini mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto siku saba; siku ya saba ni kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi.
Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; naye atautikisa mganda mbele za Bwana ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya sabato kuhani atautikisa.
Nanyi mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya sabato, tangu siku hiyo mliyouleta mganda wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia sabato saba; hata siku ya pili ya hiyo sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka ya unga mpya.
Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi mtaso- ngeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto. Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa Bwana.
Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi. Mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yo yote ya utumishi.
Sikukuu za Bwana ni hizi, ambazo mtazipigia mbiu ya kuwa ni makusanyiko matakatifu, ili mmsongezee Bwana sadaka kwa moto, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na dhabihu, na sadaka za kinywaji, kila sadaka kwa siku yake.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 8: 2-5, 9-10Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha.
Pazeni zaburi, pigeni matari,
Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda.
Pigeni panda mwandamo wa mwezi,
Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu.
K. Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha.
Kwa maana ni sheria kwa Israeli,
Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo.
Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu,
Alipoondoka juu ya nchi ya Misri;
Maneno yake nisiycmjua naliyasikia.
K. Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha.
Usiwe na mungu mgeni ndani yako;
Wala usimsujudie mungu mwingine.
Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,
Niliyekupandisha toka nchi ya Misri;
Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.
K. Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha.
Shangilio la Injili
1 The 2: 13Lipokeeni neno la Mungu, siyo kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu.
Aleluya.
Injili
Mt. 13: 54-58Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni