Jumatano ya 9 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Tob 3:1-10, 16-17Unikumbuke, unitazame; usiniadhibu kwa ajili ya dhambi zangu na makosa yangu; wala kwa ajili ya dhambi za baba zangu walioasi mbele zako.
Kwa maana hawakuzitii amri zako; kwa hiyo umetutoa tuwe mateka, hata na kuuawa; kuwa mithali ya shutumu kwao mataifa yote, ambao kwamba tumetawanyika katikati yao.
Na sasa hukumu zako zi nyingi na za kweli; hata uje unitende kwa kadiri ya dhambi zangu na za baba zangu; kwa kuwa hatukuzishika amri zako; wala kuenenda kwa kweli mbele zako. Basi sasa unitende kama uonavyo vema; uniamuru niondolewe roho yangu, ili niruhusiwe na kuwa udongo tena; maana yanifaa kufa kuliko kuishi, kwa sababu nimesikia mashutumu yasiyo haki, nami naona huzuni nyingi.
Uamuru, basi, nitolewe katika msiba huu, niende mahali pa milele; wala usiugeuzie mbali nami uso wako.
Ikawa siku ile ile huko ekbatana, mji wa Media, Sara binti Ragueli naye alishutumiwa na wajakazi wa baba yake. Maana alikuwa ameolewa na waume saba, bali Asmodeo, yule jini, aliwaua kabla hawajalala naye. Wakamwambia, Wewe hujui ya kuwa umewanyonga waume zako? Umekuwa na waume saba, wala hata mmoja wao hukupata faida naye. Mbona waturudia sisi? Ikiwa wao wamekufa, nenda zako nawe ukawafuate; tusikuone kabisa una mwana wala binti. Alipoyasikia hayo alifanya huzuni nyingi, akaona afadhali kujinyonga. Akafikiri, Mimi ni binti pekee wa baba yangu; basi nikitenda hivi nitamwita shutumu; nitamshushia uzee wake kwa huzuni hata kaburini.
Basi ikawa sala zao wote wawili zilisikiwa mbele za enzi yake Mungu Aliye juu. Rafaeli akatumwa ili awaponye wote wawili.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 25:2 – 9Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu.
Ee Mungu wangu,
Nimekutumaini Wewe, nisiaibike,
Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.
Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja;
Wataaibika watendao uhaini bila sababu.
K. Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu.
Ee Bwana, unijulishe njia zako,
Unifundishe mapito yako,
Uniongoze katika kweli yako,
Na kunifundisha.
Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu,
Nakungoja Wewe mchana kutwa.
K. Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu.
Ee Bwana, kumbuka rehema zako na fadhili zako,
Maana zimekuwako tokea zamani.
Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu,
Wala maasi yangu.
Unikumbuke kwa kadiri ya ujana wangu,
Wala maasi yangu.
Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako,
Ee Bwana, kwa ajili ya wema wako.
K. Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu.
Bwana yu mwema, mwenye adili,
Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.
Wenye upole atawaongoza katika hukumu,
Wenye upole atawafundisha njia yake.
K. Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu.
Shangilio la Injili
Mt 11:25Nakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Aleluya.
Injili
Mk 12:18-27Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni