Sikukuu ya Mt. Marko, Mwinjili
· Mwaka A
Somo la Kwanza
1Pet 5:5-14Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 89:1-2, 5-6, 15-16Fadhili zako nitaziimba milele, Ee Bwana.
Fadhili za Bwana nitaziimba milele;
Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele;
Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.
K. Fadhili zako nitaziimba milele, Ee Bwana.
Ee Bwana, mbingu zitayasifu maajabu yako,
Uaminifu wako katika kusanyiko la watakatifu.
Maana ni nani katika mbingu awezaye kulinganishwa na Bwana?
Ni nani afananaye na Bwana miongoni mwa malaika?
K. Fadhili zako nitaziimba milele, Ee Bwana.
Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe,
Ee Bwana, huenenda katika nuru ya uso wako.
Kwa jina lako hufurahi mchana kutwa,
Na kwa haki yako hutukuzwa.
K. Fadhili zako nitaziimba milele, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
1Kor 1:23-24Sisi tunamhubiri Kristu, aliyesulibiwa, ni nguvu na hekima ya Mungu.
Aleluya.
Injili
Mk 16:15-20Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni