· Mwaka C
Somo la Kwanza
Efe 1:11-14Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 33:1-2, 4-5, 12-13Heri Taifa, Mungu aliowachagua kuwa urithi wake.
Mpigieni Bwana vigelegele enyi wenye haki
Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo
Mshukuruni bwana kwa kinubi
Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa
K. Heri Taifa, Mungu aliowachagua kuwa urithi wake.
Kwa kuwa neno la Bwana lina adili
Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu
Huzipenda haki na hukumu
Nchi imejaa fadhili za Bwana
K. Heri Taifa, Mungu aliowachagua kuwa urithi wake.
Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao
Watu waliochaguliwa kuwa urithi wake
Toka mbingu bwana huchungulia
Huwatazama wanadamu wote pia
K. Heri Taifa, Mungu aliowachagua kuwa urithi wake.
Shangilio la Injili
Zab 147:12-15Msifuni bwana, Ee Yerusalemu
Huipeleka amri yake juu ya nchi
Aleluya.
Injili
Lk. 12:1-7Name nawaambia ninyi rafiki zangu, msiwaogope hao wauuao mwili, kisha baada ya hayo hawana wawezalo kutenda Zaidi. Lakini nitawaonya mtakayemwogopa, mwogopeni yule ambaye akiishakumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanam; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo. Je! Mashomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu. Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi, bora ninyi kuliko mashomoro wengi.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni