Jumatatu ya 7 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ybs 1:1–10Hekima iliumbwa kabla ya vitu vyote, na ufahamu wa busara tangu milele. Nani aliyefunuliwa shina la hekima? Nani aliyejua mashauri yake merevu? Yuko mmoja aliye na hekima, naye yu wa kuogopwa sana, ameketi katika kiti chake cha enzi. Bwana ndiye aliyeiumba na kuiona na kuihesabu, na kumwaga juu ya kazi zake zote. Ina wote wenye mwili kama aitoavyo, na wale wampendao amewapa kwa wingi.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 93:1–2, 5Bwana ametamalaki, amejivika adhama.
Bwana ametamalaki, amejivika adhama,
Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. (K)
K. Bwana ametamalaki, amejivika adhama.
Naam, ulimwengu umethibitika isitikisike;
Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani;
Wewe ndiwe uliye tangu milele. (K)
K. Bwana ametamalaki, amejivika adhama.
Shuhuda zako ni amini sana;
Utakatifu ndio uifaao nyumba yako,
Ee Bwana, milele na milele. (K)
K. Bwana ametamalaki, amejivika adhama.
Shangilio la Injili
Zab 27:11Ee Bwana, unifundishe njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.
Injili
Mk 9:14-29Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni