Jumanne ya 6 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mwa 6:5–8, 7:1–5, 10Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki. Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke. Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote. Kwa maana baada ya siku saba nitainyesha dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wan chi nitakifutilia mbali. Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru.mIkawa baada ya siku hizo saba, maji ya gharika yakawa juu ya nchi.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 29:1–4, 9–10Bwana atawabariki watu wake kwa Amani.
Sauti ya Bwana, enyi wana wa Mungu,
Mpeni Bwana utukufu na nguvu;
Mpeni Bwana utukufu wa jina lake;
Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.
K. Bwana atawabariki watu wake kwa Amani.
Sauti ya Bwana I juu ya maji,
Bwana yu juu ya maji mengi
Sauti ya Bwana ina nguvu,
Sauti ya Bwana ina adhama.
K. Bwana atawabariki watu wake kwa Amani.
Sauti ya Bwana yawazalisha ayala,
Na ndani ya hekalu lake wanasema wote, Utukufu.
Bwana aliketi juu ya Gharika;
Naam, Bwana ameketi hali ya mfalme milele.
K. Bwana atawabariki watu wake kwa Amani.
Shangilio la Injili
Zab 25:4–5Ee Bwana, unijulishe njia zako, unifundishe mapito yako.
Aleluya.
Injili
Mk 8:14–21Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni