Ijumaa ya 3 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ebr 10:32-39Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 37:3-6, 23-24, 39-40Wokovu wa mwenye haki una Bwana.
Umtumaini Bwana ukatende mema,
Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.
Nawe utajifurahisha kwa Bwana,
Naye atakupa haja za moyo wako.
K. Wokovu wa mwenye haki una Bwana.
Umkabidhi Bwana njia yako,
Pia umtumaini, naye atafanya.
Ataitokeza haki yako kama nuru,
Na hukumu yako kama adhuhuri.
K. Wokovu wa mwenye haki una Bwana.
Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana,
Naye aipenda njia yake.
Ajapojikwaa hataanguka chini,
Bwana humshika mkono na kumtegemeza.
K. Wokovu wa mwenye haki una Bwana.
Na wokovu wa wenye haki una Bwana;
Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.
Naye Bwana huwasaidia na kuwaopoa;
Huwaopoa na wasio haki na kuwaokoa;
Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.
K. Wokovu wa mwenye haki una Bwana.
Injili
Mk 4:26-34Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni