Jumatatu ya 27 ya Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Gal. 1:6 – 12Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 111:1 – 2, 7 – 10Alikumbuka agano lake milele.
Aleluya.
Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote,
Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
Matendo ya Bwana ni makuu,
Ukawafunulia watoto wachanga.
K. Alikumbuka agano lake milele.
Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu,
Maagizo yake yote ni amini.
Yamethibitika milele na milele,
Yamefanywa katika kweli na adili.
K. Alikumbuka agano lake milele.
Amewapelekea watu wake ukombozi,
Ameamuru agano lake liwe la milele.
Jina lake ni takatifu la kuogopwa.
Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima,
Wote wafanyao hayo wana akili njema,
Sifa zake zakaa milele.
K. Alikumbuka agano lake milele.
Shangilio la Injili
2Kor. 5:19Mungu alikuwa ndani ya Kristo,
akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake,
ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Aleluya.
Injili
Lk. 10:25-37Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani? Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipitia kando. Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapitia kando.
Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na lipomwona alimhurumia, akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na chochote utakachogharimiwa Zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.
Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake, yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi? Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni