Ijumaa ya 1 ya Majilio
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 29:17-24Basi, Bwana aliyemkomboa Ibrahimu asema hivi, katika habari za nyumba ya Yakobo; Yakobo hatatahayarika sasa, wala uso wake hautabadilika rangi yake. Basi atakapowaona watoto wake, walio kazi ya mikono yangu, katikati yake, wao watalitakasa jina langu; naam, watamtakasa Mtakatifu wa Yakobo, nao watamcha Mungu wa Israeli. Hao nao wakosao rohoni mwao watapata kufahamu, na hao wanung’unikao watalifunza elimu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 27:1,4,13-14Bwana ni nuru ya wokovu wangu.
Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu,
Nimwogope nani?
Bwana ni ngome ya uzima wangu,
Nimhofu nani?
K. Bwana ni nuru ya wokovu wangu.
Neno moja nimelitaka kwa Bwana,
Nalo ndilo nitakalolitafuta,
Nikae nyumbani kwa Bwana,
Siku zote za maisha yangu.
Niutazame uzuri wa Bwana,
Na kutafakari hekaluni mwake.
K. Bwana ni nuru ya wokovu wangu.
Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana,
Katika nchi ya walio hai.
Umngoje Bwana, uwe hodari,
Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.
K. Bwana ni nuru ya wokovu wangu.
Shangilio la Injili
ShangilioTazama Bwana wetu atakuja na nguvu, Na atayaangaza macho ya watumishi wake.
Aleluya.
Injili
Mt 9:27-31Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni