Jumanne ya 34 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ufu 14:14–19Kisha malaika mwingine akatoka katika lile hekalu lililoko mbinguni, yeye naye ana mundu mkali. Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sansa. Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 96:10–13Bwana atauhukumu ulimwengu kwa haki.
Semeni katika mataifa, Bwana ametamalaki;
Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike,
Atawahukumu watu kwa adili.
Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie,
Bahari na ivume na vyote viijazavyo.
K. Bwana atauhukumu ulimwengu kwa haki.
Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo,
Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha;
Mbele za Bwana, kwa maana anakuja,
Kwa maana anakuja aihukumu nchi.
Atauhukumu ulimwengu kwa haki,
Na mataifa kwa uaminifu wake.
K. Bwana atauhukumu ulimwengu kwa haki.
Shangilio la Injili
Yak 1:21Pokeeni kwa upole neno la Mungu, lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Aleluya.
Injili
Lk 21:5-11Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni