Alhamisi ya 29 na Mwaka
· Mwaka C · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Efe 3:14–21Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu, naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 33:1–2, 4–5, 11–12, 18–19Nchi imejaa fadhili za Bwana.
Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki,
Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
Mshukuruni Bwana kwa kinubi,
Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.
K. Nchi imejaa fadhili za Bwana.
Kwa kauwa neno la Bwana lina adili,
Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
Huzipenda haki na hukumu,
Nchi imejaa fadhili za Bwana.
K. Nchi imejaa fadhili za Bwana.
Shauri la Bwana lasimama milele,
Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
K. Nchi imejaa fadhili za Bwana.
Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao,
Wazingojeao fadhili zake.
Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,
Na kuwahuisha wakati wa njaa.
K. Nchi imejaa fadhili za Bwana.
Shangilio la Injili
Yn 17:17Neno lako ndiyo kweli, Ee Bwana, ututakase kwa ile kweli.
Aleluya.
Injili
Lk 12:49-53Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni