Jumanne ya 27 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Gal 1:13–24Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 139:1–3, 13–14Uniongoze, Ee Bwana, katika njia ya milele.
Ee Bwana umenichunguza na kunijua.
Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;
Umelifahamu zazo langu tokea mbali.
Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,
Umeelewa na njia zangu zote.
K. Uniongoze, Ee Bwana, katika njia ya milele.
Niende wapi nijiepushe na roho yako?
Niende wapi niukimbie uso wako?
Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko;
Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
K. Uniongoze, Ee Bwana, katika njia ya milele.
Ningezitwaa mbawa za asubuhi,
Na kukaa pande za mwisho za bahari;
Huko nako mkono wako utaniongoza,
Na mkono wako wa kuume utanishika.
K. Uniongoze, Ee Bwana, katika njia ya milele.
Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,
Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa
Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.
K. Uniongoze, Ee Bwana, katika njia ya milele.
Shangilio la Injili
Yn 14:5Bwana anasema: mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Aleluya.
Injili
Lk 10:38-42Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni